Mchungaji Kilinda- Mtaa wa Shinyanga Mjini |
Shinyanga Adventist Sec School |
Hii picha inaonyesha majengo ya madarasa ya Shinyanga Adventist secondary school iliyopo Ndala, Manispaa ya Shinyanga inayoendelea kujengwa na hapa ndipo ile semina ya mafunzo ya kufyatua matofali kwa udongo wa kawaida ukichanganya na simenti mfuko mmoja wa simenti unakupatia zaidi ya matofali mia moja.
Wachungaji tumeni washiriki waje ili tujifunze namna ya kufyatua matofali mazuri na imara. Chakula kitapatikana eneo la mkutano kuanzia gharama ya Tshs 3,000/= na kuendelea. Tunawakumbusha walio na mahema (tents) waje nayo ili kupunguza gharama za kuishi.
Eneo la wazi la shule |
Usafiri kutoka Shinyanga Mjini kwa pikipiki ni kati ya Tshs 1,500 na 2,000. Pia ukipenda kutumia usafiri wa baiskel ni maelewano na tunaposema usaifir wa baiskeli inatokana na uwepo wa baiskeli nyingi kuliko gari. Nyumba za wageni yaani 'guest house' ziko jirani na eneo la semina na zinapatikana kwa Tsh 5000 na kuendelea hadi 120,000. Semina ni ya kujitegemea kwa kila kitu.
Barikiweni mnapojipanga kuja.
Tangazo hili limetolewa na Mchungaji J.J Kilinda
Mchungaji wa Mtaa wa Shinyanga Mjini
Post a Comment