
Kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini inatarajiwa kuzindua mkanda wake wa tatu mnamo tarehe 02 Aprili 2017 kuanzia saa 06 mchana. Uzinduzi wa mkanda huu utafanyika katika viwanja vya kanisa la Shinyanga Mjini. Nyimbo za mkutukuza Mungu zitaimbwa ambapo Kwaya na vikundi mbalimbali vya uimbaji ndani ya Manispaa ya Shinyanga wamealikwa.

Mnaalikwa kushuhudia tukio hili la kipekee. Hakuna kiingilio chochote na lango kuu la kuingia katika viwanja vya kanisa litakuwa wazi kuanzia asubuhi saa 12. Unaomwa kualika ndugu, jamaa na marafiki.
Mungu akubariki unapopanga kuja kwenye tukio hili la kipekee. Pia panga kuchukua nakala yako kwa ajili ya kusikiliza mara baada ya kubariki mkanda huu.
Post a Comment