Ruth Ng'washi (Mrs Maeja) |
WIMBO: NAMBA 125-Uniangalie atwambia Yesu aliyetufia
"Tukiwa tunajiandaa na meza ya Bwana Jumamosi tarehe 01 April 2017, tujitathimini katika kitabu cha Zaburi 14:2 ambapo tunapata ujumbe wa jinsi Mungu anatuona. Wote tunahesabika ni wadhambi lakini kupitia kifo cha Yesu kristo kila mmoja amepata nafasi ya kurithi Ufalme wa Mungu.
Tunapo tafakari kwa muda wa juma hili, tutagundua kuwa muda mwingi tumeutumia kutafuta pesa. Neno la Bwana siku ya leo linatufundisha kumtafuta Mungu kwa bidii. Tutakapomtafuta Mungu kwa bidii, mambo mengine atatupatia.
Sote kama wadhambi tunaleta toba yetu kwa Mungu mwenye huruma na upendo. Tunapoomba toba mungu wetu mwaminifu hutupatia nafasi nyingine ya kipekee zaidi ya kuujua ukuu wake. kwa kutafakari mambo ambayo hayako sawa kutasaidia kuomba msamaha kwa Mungu wetu. Kila mmoja wetu aombe toba binafsi ya kupata kibali ili ibada yetu ya Meza ya Bwana ipokelewe kwa utukufu wa Mungu."
BWANA ATUBARIKI SOTE
+ comments + 1 comments
Ubarikiwe na bwana
Post a Comment