Mchungaji wa Mtaa wa Shinyanga Mjini, Mch. Joram Kilinda amewakabidhi vijana watafuta njia kama ishara ya kuwapatia majukumu ya kuongoza katika kufanya kazi ya Mungu.
Kwa ushawishi wa vijana walionao, vijana ni kundi ambalo linahitaji motisha na kutiwa moyo kutoka kwa wazazi na walezi. Kwa kutumia akili zao, nguvu zao za kimwili na kiroho hawataweza kushindwa na mbinu za shetani.
Makabidhiano hayo ya bendela ni mwanzo wa kuanza masomo ambayo watafunzwa mafundisho mbalimbali kwa lengo la kuhitimu na kupewa tuzo za nishani mbalimbali katika mkutano mkuu utakaofanyika Mkoani Iringa mwezi Desemba 2017.
Pia wakati wakionyesha programu zao kanisani, Vijana Watafuta Njia (Path Finder-PC ) wametoa wito wa kulaani vitendo vya kihuni na kuwataka washiriki na wananchi kiujumla kutofumbia mambo vitendo vinavyochangia maambukizi ya Virusi vinavyosababisha UKIMWI.
Wito huo ulitolewa wakati wakiwasilisha programu yao maalumu wakati wa mchana baada ya ibada ya asubuhi. Sabato ya leo ilikuwa maalumu kwa vijana wote walio katika kanisa la Shinyanga Mjini.
Wakati huo huo Mch. Kilinda ametoa wito kwa wazazi na washiriki kuwaleta watoto wao kanisani na waweze kujiunga na chama cha vijana ili waweze kupata mafundisho mbalimbali ambayo yatawajenga kiakili, kiroho na kimwili.
"Wazazi wenzangu tunatakiwa kutumia elimu iliyopo kanisani ili kuwalea watoto wetu, wazazi mtuamini tuwafundishe watoto wetu ili wawe raia bora katika ulimwengu huu na kwa kanisa" Alisema Mchungaji Kilinda.
Post a Comment