Kanisa la Waadventista wa Sabato limetakiwa kubadilisha namna ya kufahamika katika vitu vyote inavyotumika mahali popote duniani. Wito huo umetolewa na Mchungaji Samuel Neves ambaye ni Mkurugenzi mwenza wa Mawasiliano Duniani wa Kanisa la Wasabato. Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa GAIN katika ukumbi wa mikutano wa NSSF Mwanza, aliwakumbusha kuwa kanisa la Waadventista wa Sabato lina jumla ya makanisa zaidi 150,000 katika nchi 208 lakini halijulikani kutokana na kutokuwa na utambulisho maalumu kama ilivyo katika makampuni binafsi kama vile kampuni ya Nike na McDonald. Akitolea mifano ya nembo mbalimbali zinazotumika na kanisa zinachangia kwa kiasi kikubwa kutotambulika kwa kanisa. Baadhi ya nembo hizo ni kama vile nembo za vyama mbalimbali vilivyopo katika kanisa kama vile Chama cha watafuta njia, chama cha wavumbuzi, chama cha vijana wakubwa, umoja wa wanamitandao. |
| | | |
|
|
Mchungaji Brent Hardinge |
|
Mchungaji Samuel Neves |
Wakati huo huo Mchungaji Brent Hardinge ambaye pia ni Mkurugenzi mwenza wa mawasiliano wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani ametoa wito kwa watengeneza tovuti za kanisa, kutumia mfumo mmoja wenye muonekano unaofanana ambao utasaidia kulitambulisha kanisa katika tasnia ya mifumo ya kimtandao. Alisema kuwa mfumo huo ni huru kwa mtumiaji yeyote na hauna gharama zozote. Aliutaja mfumo huo ambao kanisa limeamua kuutengeneza umaitwa ALPS yaani Adventist Living Pattern system.
|
Mchungaji Jonatan Conceicao |
Post a Comment