 |
Kutoka kushoto ni Gedion Msambwa, Christopher Ungani na Mch. Malekana |
 |
Mchungaji Mark Malekana-President STU |
"Nimezaliwa karibu na mto Simiyu, nikakulia katika mto Duma. Ukiingia kwenye mto uliojaa na usipofuata utaratibu wake kwa kuheshimu mkondo wake. Maji ya mto yakiona unang'ang'ana na hutaki kufuata utaratibu wake yatakuzamisha kwanza ili upate adabu. halafu yanakugeuza geuza na iwapo yamekuzamisha na bado hujaelewa somo, yanakuua. Halafu ukifa ndo unaelea juu ya maji ili uonekane kuwa yamekuua. Halafu ikielea ndipo yanakupeleka ziwani na hayakosei kukufikisha ziwani nsa yanatafuta mahali palipo na gravity kubwa yanakuweka hapo kwenye 'hashosho'" Maneno haya yamenenwa na Mchungaji Mark Malekana wakati alipokuwa akiwapongeza kwa kazi nzuri iliyofanywa na Gedion Msambwa na Christopher Ungani ambao ni Wakurugenzi wa Mawasiliano katika ngazi ya Union ya kaskazini na ile ya Kusini mwa Tanzania kwa kufanikiwa kwa kiwango cha juu kufanyika kwa mkutano mzuri sana wa GAIN jijini Mwanza.
 |
Kutoka kushoto ni Gedion Msambwa, Christopher Ungani na Mch. Malekana |
Katika mfano wa mto alieleza kuwa alikuwa na ujumbe kwa viongozi kufanya kazi kwa namna ambayo Mungu ameruhusu kazi itendeke. Mkondo wa maji wa sasa unahitaji matumizi ya TEHAMA katika injili ya siku za mwisho. Aliwashauri viongozi wanaong'ang'ania njia za zamani, kuwa watajikuta wako ni wachache ndani ya kanisa na vijana ambao ndiyo kasi ya mkondo wa maji ya mto watajikuta wamewaacha wazee hao katika eneo moja aliloliita "shosho".
Post a Comment