Mchungaji Musa Mika-Website and Apps Manager Ufunuo Publishing House |
Kufikia mwaka 2020 inakadiriwa kuwa zaidi ya vifaa bilioni 20 hadi 100 kuunganishwa katika mtandao mmoja unaojulikana kama 'Internet of Things'. Hato yameelezwa leo na Mchungaji Musa Mika (Website and Apps Manager-Ufunuo Publishing House) wakati akiwasilisha mada ya matumizi ya machapisho ya kimtandao dhidi ya machapisho yaliyopo katika karatasi. 'Kama unadhani Intaneti imekusaidia kubadilisha maisha yako, basi jiandae kubadilishwa maisha yako zaidi kwa ujio wa mtandao wa vitu ('Internet of Things')'. Alisema Mchungaji Musa Mika.
Aliendelea kusema kuwa waumini wategemee mabadiliko ya kasi ya ulimwengu kwa sababu wanadamu wataunganishwa kwa pamoja, vitu kwa vitu vitaunganishwa na wanadamu kwa vitu pia vitaunganishwa ili kutengeneza mtandao mkubwa sana. Utakuwa ni ulimwengu ambao mwanadamu ataweza kuchemsha chai, kahawa na mabo mbalimbali akivitawala vifaa vyake vya nyumbani au ofisini akiwa mbali na maeneo yake nyumbani au ofisini.
Mchungaji Musa Mika |
Wakati huo huo aliwataka waumini wawapo kanisani, kuhakikisha kuwa simu zao ziko katika hali ya utulivu wanapokuwa wakijisomea maandiko matakatifu kama vile lesoni. Pia simu ni vema iwe katika mwanga hafifu ambao hautamuathiri muumini mwenzake aliyekaribu na mtumiaji wa simu. Akisisitiza matumizi sahihi ya simu kanisani aliendelea kusema kuwa mtumiaji wa simu lazima azime sauti zote za ishara ya ujumbe wowote kuingia,hii itasaidia kutoharibu usikivu katika ibada. Kwa kuandaa apps ambazo utazitumia, itasaidia sana kuongeza usikivu.
Post a Comment