Mchungaji David Makoye |
Mchungaji David Makoye |
Mchungaji David Makoye ambaye ni Katiku Mkuu wa Union ya Kaskazini mwa Tanzania, amelitaka kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania kutumia fursa ya mabadiliko ya Teknolojia Habari na Mawasiliano kusambaza ujumbe wa Yesu Kristo kwa kasi na kwa haraka. Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa GAIN unaondelea katika ukumbi wa NSSF Mwanza Tanzania, Mchungaji Makoye amewaomba wana mawasiliano kutumia mitandao ya kijamii kwa ubora, salama na kwa usahihi. "Tatizo si mitandao ya kijamii kwa jamii ya leo. Tatizo ni jamii kuelewa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii" Alisema Mchungaji Makoye.
Wakati huo huo Mchungaji Makoye ameyaomba makanisa mahalia kuweka kwenye mipango ya bajeti, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA ikiwemo Kompyuta, Tabiti, Kamera ili kufanikisha nia ya kutumia mitandao ya kijamii kueneza injili kwa lengo la kutimiza agizo la Yesu Kristo la kuwafanya watu wote duniani kuwa wanafunzi wa Yesu.
Post a Comment