![]() |
Kanisa la Waadvenstista wa Sabato Masoko |
Watu wasiofahamika, wanaosadikika kuwa majambazi usiku wa kuamkia leo wamevamia na kusababisha uhabifu mkubwa ndani ya Kanisa la Waadvenstista wa Sabato Masoko, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Watu hao wamechimba shimo lenye upana wa futi sita na kina cha futi sita katika eneo la mimbari ya kanisa kwa kile kinachohisiwa kutafuta hazina au vito vilivyoachwa na wajerumani.
![]() |
Shimo lililochimbwa ndani ya kanisa |
Uvumi huu umelisababishia kanisa hili hasara kubwa na kuliweka kanisa katika hali ya hatari kwa sababu hivi karibuni kanisa limefanya ukarabati mkubwa wa takribani TSH 100Mil, ikiwa ni matengenezo juu ya kanisa la awali lililojengwa miaka 50 iliyopita.
Wataalam wa madini toka Wilaya ya Rungwe walishafika katika eneo hili na kupima na kuonyesha kuwa eneo hilo halina hazina wala madini yoyote zaidi ya miamba iliyopo na kuwasihi watu kuachana na imani potofu ambayo inalisababishia kanisa hasara wakati wa matukio kama haya.
Kanisa la Waadventista wa Sabato Masoko ndilo kanisa kongwe kabisa katika mikoa ya nyanda za juu kusini kwa kanisa la waadventista wasabato, likiwa limejengwa na wazawa mwaka 1967, takribani miaka 49 baada ya Wajerumani kuondoka nchini. Hakuna ushahidi wowote kuwa Wajeruman waliwahi kufika eneo la Masoko kipindi chote ch autawala wao 1886-1918.
![]() |
Mahali amabapo palikuwa na kengere kubwa, wezi wameiiba wakidhani kuwa nimojawapo ya hazina |
![]() |
Shimo ndani ya kanisa lililochimbwa na wezi |
Post a Comment