 |
| Mzee Kasonzo Washington akimlisha keki mke wake |
FUNGU KUU:
“MPENZI NAOMBA UFANIKIWE KATIKA MAMBO YOTE
NA KUWA NA AFYA YAKO, KAMA ILE ROHO YAKO IFANIKIWAVYO” 3 YOHANA 1:2
Sabato ya leo iliabudiwa kwa kicho na kisha wanandoa waliohudhuria ibada walipata nafasi ya kulishana keki kama ishara ya kukumbuka tukio la siku walipoona. Ibada ya leo ilikuwa ni hitimisho la juma la kaya na familia ambalo somo kuu lilikuwa katika kuhamasisha wanandoa kuishi katika viapo vyao.
 |
| Ndugu Raphael na mke wake wakilishana keki |
 |
| Ndugu Sarya na mke wake wakilishana keki |
WAZO KUU
Mungu ametoa baadhi ya kanuni rahisi za
kinga ambazo huweza kusaidia wanandoa kudumisha afya ya ndoa zao.
NI KWANINI NDOA INAHITAJI KINGA.
Hebu angalia mfano huu
1.
Mwana-sayansi mmoja aliwahi
kusema kwa kila kijiko kimoja cha udongo wa bustani anakadiria kuwa kuna viumbe
milioni 500
2.
Kwamba nusu kijiko cha mate
kina bilioni moja ya viumbe visivyoonekana.
Wakati baadhi ya vijidudu na bakteria hawa
wana madhara, lakini wengi wao hawana madhara.
Kuzungumzia mifano hiyo miwili mwandishi
ametoa mfano wa kile wanachofanya wanaharusi kati nchi hizi za magharabi pale
mchungaji anapomwambia bwana harusu “
SASA UNAWEZA KUMBUSU BIBI HARUSI” Wenzi hao hushiriki zaid ya upendo.
Wanachofanya ni kubadilishana majeshi mengi sana ya viumbe hai.
Ona hili. Tunaishi katika mazingira yenye
uwadui na sisi kwa hali ya kimwili, kiroho na kimahusiano. Kirusi au bakteria
mkubwa ni dhambi na maelfu ya kiutendaji.
Ndoa ambayo ni uhusiano wa karibu wa
familia mara nyingi ni rahisi kushambuliwa.
Mkakati uliotayarishwa na shetani mwenyewe
kuingiza katika ndoa aina Fulani ya ugonjwa unao ua.
Waweza kusikiliza ushuhuda wa wazee katika ndoa zao katika sehemu ya video zetu au bonyeza hapa kwenda kwenye akaunti yetu ya youtube
 |
| Ndugu Eliud Misana na mke wake wakilishana keki |
 |
| Dr Maeja na mke wake wakilishana keki |
 |
| Mzee Kasonzo akichukua keki kwa ajili ya kumlisha mke wake ambaye hayupo katika picha kutokana na maradhi. |
 |
| Mzee wa kanisa ndugu Songola na mke wake wakilishana keki |
 |
| Mwalimu Magoma (mkuu wa kaya na familia) na Mke wake wakilishana keki |
 |
| Mzee Geofrey Mndambi na mke wake (Wageni wa kanisa) wakiwa mbele kwa ajili ya kulishana keki. Walioana mwaka 1960 na wamekuwa msaada mkubwa kushuhudia maisha yao ya ndoa |
 |
| Mzee wa kanisa ndugu Sengoka Mndambi akihubiri wakati wa huduma kuu |
 |
| Ndugu Raphael na mke wake wakiwa mbele ya kanisa wakiwa katika muonekano wa kuwa pamoja kanisani |
 |
| Ndugu Songola (Mzee wa Kanisa) na mke wake wakitambulishwa kanisani wakionyesha mfano wa kuwa pamoja kwa wanandoa kanisani |
 |
| Mzee wa kanisa ndugu Sengoka Mndambi akitambulisha familia ya Mwalimu Magoma (Mkuu wa kaya na familia kanisani) |
 |
| Washiriki wa kanisa wakiwa katika ibada |
 |
| Washiriki wa kanisa wakiwa katika ibada |
 |
| Kwaya ya wanadoa wakiimba wimbo wakati ibada kuu |
 |
| Mzee Mndambi na mke wake wakiimba wimbo wakati wa ibada kuu |
 |
| Wanandoa wakiimba wimbo wakati wa ibada kuu |
 |
| Wanandoa wakiimba kwa furaha (anayetabasamu ni mama Yuritha Nangare na anayeongoza kwaya ya wanandoa ni mzee Samweli Mboje) wakati wa ibada kuu |
 |
| Ndugu Peter Stima akisoma somo la sadaka wakati wa kutoa zaka na sadaka |
Post a Comment