Watoto wakimsikiliza mwalimu wao katika ibada yao kanisani. Walimu wameendelea kutoa mafundisho kwa watoto wote kwa njia mbalimbali ikiwemo kuimba, kuangalia picha.
PFC kutoka kanisa la Ndala wakiwa katika gwaride ambalo linaonesha ukakamavu wao katika kazi ya Bwana Yesu.
Mchungaji Elias Switta akihubiri katika ibada kuu ya mchana wa Jumatano 06 Julai 2016. Watu wameendelea kujitoa kwa Yesu na wanajiandaa kwa ubatizo mkubwa utakaofanyika ijumaa 08 Julai 2016
Vijana wakiwa katika darasa lao linawajumuisha vijana wote ambao hawajaingia katika dola ya ndoa, Vijana wameendelea kupata masomo mazuri kama vile namna ya kumoata mwenzi wa maisha, usafi na utii.
Bwana Mackdonald kutoka kanisa la Nyakato(Muimbaji) akichangia katika darasa la vijana namna ya kupata mwenzi wa maisha.
Anna Mdongo (Kijana) kutoka kanisa la Shinyanga Mjini akichangia katika darasa la vijana namna ya kupata mwenzi wa maisha.
Bi Anneth kutoka kanisa la Nyakato(Muimbaji) akichangia katika darasa la vijana namna ya kupata mwenzi wa maisha.
Mchungaji Tobe (Mchungaji wa Mtaa wa Lubaga) akifundisha namna ya kupata mwenzi wa maisha katika darasa la vijana
Post a Comment