Home » » 37 WABATIZWA TMI

37 WABATIZWA TMI

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Saturday, July 01, 2017 | July 01, 2017

 Mchungaji Joram Kilinda --Mchungaji wa Mtaa wa Shinyanga akibatiza waliojitoa katika Mahubiri ya TMI

Jumla ya watu 37 wamebatizwa katika mahubiri ya TIM (Total Member Involvement), mahubiri ambayo yalianza Juni 11 2017 na yamehitishwa leo ambapo leo Jumamosi watu 21 wamejitoa na kubatizwa. Ubatizo wa leo ni wa pili kufanyika ukitanguliwa na ubatizo uliofanyika Jumamosi ya Juni 24 2017 na jumla wa watu 16 walibatizwa.


 Jumla ya watu 21 wakiapishwa na kusema ahadi ya ubatizo kabla ya ubatizo leo

Kanisa la Shinyanga Mjini limekuwa na vituo viwili katika eneo la Misufini lililopo katika Kata ya Ndala na kituo cha Kitangili katika kata ya Kitangili. Vituo vyote viwili vilihudumiwa na Idara ya Vijana kupitia kwaya ya Vijana katika kituo cha Kitangili na Kwaya ya Kanisa (Shinyanga Adventist Choir- SAC) katika kituo cha Misufini. Pia wanachama wa chama cha watafuta njia (Path Finder-PF) walishiriki kwa namna ya kipekee ya kuonyesha gwaride ikiwa ni mbinu ya kufanya mialiko kwa watu kuja kusikiliza ujumbe wa Yesu Kristo ambao ulinenwa kupitia Wachungaji Saimoni Magesa (Kituo cha Misufini) na Yona Nguno (Kituo cha Kitangili).

 Waumini wakimsikiliza Mchungaji Yona wakati wa Ibada Kuu kabla ya Huduma ya Ubatizo wa watu 21 Kufanyika.

Wakati huo huo katika ibada ya Sabato ambayo iliongozwa na Mchungaji Yona Nguno, amesema kuwa kwa sasa tunaishi katika wakati rehema ya Mungu ambayo sauti ya Mungu inawaita watu wake wamrudie mapema ili kujiandaa na ujio wa Yesu Kristo kwa mara pili. Pia amewataka waumini wapya waliobatizwa katika mahubiri ya TMI kuweza kuwa waaminifu kwa Mungu kwa kufuata maandiko matakatifu waliyoamini, ili waweze kuwa watu wema kwa jamii, taifa na kwa Mungu."Japo shida zaweza kuwaandama mara baada ya kuamini na kubatizwa, lakini nawaambieni Mungu atakuwa nanyi siku zote na msikate tamaa. Wakati fulani changamoto zaweza kuwapata hata ndani ya waumini wa kanisa hili hili mliloliamini na kulikubali, lakini tambueni Mungu anawaona na kuwalinda" Amesema Mchungaji Yona.


Kwaya ya Vijana wakiimba wakati wa huduma ya kutoa zaka na sadaka

Mke wa Mchungaji Saimon Magesa akisalimia Mkutano. Kushoto ni Mchungaji Saimoni Magesa aliyehubiri kituo cha Misufini 
 
Mchungaji Yona Nguno akihubiri wakati wa Huduma Kuu leo
 
Kwaya ya Kanisa la Shinyanga Mjini wakiimba wakati wa Huduma Kuu kabla ya Mchungaji Yona Kusimama na kunena neno la Mungu

 Waumini wapya wakisema kiapo na ahadi ya ubatizo kabla kubatizwa. Ubatizo huu ni matokeo ya mahubiri ya TMI yaliyofanyika katika vituo viwili.
Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger