Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa la Waadventista wa Sabato Kanda ya Kaskazini Dr. Godwin Lekundayo ameweka jiwe la msingi katika jengo la utawala la shule ya sekondari ya kiadventista ya Shinyanga ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Januari 2018. Dr Lekundayo aliambatana na Askofu Mkuu wa Jimbo la Kusini mwa Nyanza Mch. Sadock James Butoke na Mkurugenzi wa Elimu wa Jimbo la Kusini mwa Nyanza Mwl.Isaacks Manyonyi.
Dr Godwin Lekundayo akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi
Dr Lekundayo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao
katika shule za kanisa la waadventista wa Sabato ili waweze kupata elimu
bora itakayowasaidia watoto wao kuwa raia bora kwa taifa na kisha kuwa
na kuwa na hakika ya kuurithi ufalme wa mbinguni wakati wa ujio wa Yesu
Kristo kwa mara ya pili. Pia Dr Lekundayo amependekeza kanisa kuwa shule ya kanisa ya vipaji maalumu kwa kila mkoa ili ziweze kuwa mfano kwa shule nyingine. "Ninapenda kuwapongeza kwa ujenzi wa shule lakini pia ninatoa wito wa kuendelea kujitoa kwa ajili ya kuendelea kujenga shule nyingi sehemu mbalimbali" Alisema Dr Lekundayo.
Dr. Godwin Lekundayo akiongea mbele ya washiriki kutoka makanisa ya mtaa wa Shinyanga Mjini
Kabla ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la utawala, Dr Lekundayo alikagua gwaride la vijana wa chama cha watafuta njia kutoka kanisa la waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini ambapo aliwashukuru vijana hao kwa kuendelea kulitumikia kanisa. Wakati akitembelea eneo la shule ili kuona maeneo ya shule, Dr Lekundayo ametoa wito kwa makanisa na taasisi zake za Elimu na Afya kuyalinda maeneo yake kwa kuyawekea uzio unaotambulisha mipaka yao. Ametoa wito huo mara baada ya kupokea taarifa ya kuvamiwa sehemu ya eneo la shule, taarifa ambayo imemlazimu kuwaomba waumini kuendana na kasi ya uendelezaji wa maeneo ya kanisa.
Jengo la Utawala la shule ya Sekondari ya Shinyanga Adventist
Naye Mkurugenzi wa Elimu wa Jimbo la Nyanza Kusini Mwl.Isaacks Manyonyi amewaeleza washiriki wa Kanisa Kanda ya Shinyanga kuwa kwa sasa kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo la Nyanza Kusini lina mkakati wa kuhakikisha kila mkoa kuwa na Shule ya Sekondari na Shule za Msingi. "Kwa siku nyingi mkoa wa Shinyanga na mkoa wa Geita ndiyo mikoa pekee ambayo kanisa la Waadventista wa sabato hawakuwa na shule ya sekondari. Idara ya Elimu Jimbo la Nyanza Kusini tumekuwa na mkakati wa kuwa na shule mbili kufikia mwaka 2018 ambazo ni Shinyanga Adventist Secondary School yenye mchepuo wa masomo ya Sayansi na kule Geita kutakuwa na Uzinza Adventist Secondary School." Alisema Mwl Isaacks Manyonyi.
Kutoka kulia ni Mwl. Isaacks Manyonyi (Mkurugenzi wa Elimu-SNC), Dr Godwin Lekundayo(Askofu Mkuu Jimbo la Tanzania-Kanda ya Kaskazini), Mzee Kanakoko (M/Kiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule) na Mch. Kilinda (Mchungaji Mtaa wa Shinyanga)
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga unaendelea kwa michango ya nguvu na mali ya wadau mbalimbali wa maendeleo kanda ya Shinyanga wakiwemo vijana na kwaya mbalimbali za Shinyanga ambao wameshiriki kujitoa kutengeneza matofali yanayotumika kujengea jengo la utawala.
PFC Shinyanga Mjini wakitoa heshima kwa mgeni rasmi Dr Godwin Lekundayo
PFC Shinyanga Mjini wakiwavisha Dr Godwin Lekundayo (kushoto) na Mch. Sadock Butoke- Askofu Mkuu SNC)
Washiriki wa kanisa kutoka mtaa wa Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mgeni Rasmi
Washiriki wa kanisa kutoka mtaa wa Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mgeni Rasmi
PFC wakimsikiliza mgeni rasmi
Washiriki wa kanisa kutoka mtaa wa Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mgeni Rasmi
Washiriki wa kanisa kutoka mtaa wa Shinyanga Mjini wakimsikiliza Mgeni Rasmi
PFC wakimsikiliza mgeni rasmi
Post a Comment