Home » » NJOO YESU AKUFUMBUE MACHO

NJOO YESU AKUFUMBUE MACHO

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Monday, July 17, 2017 | July 17, 2017

 Mchungaji Robert Tvako- Mfasiri Ufunuo Publisher (Morogoro)

Mchungaji Robert Tvako leo jioni ametoa wito kwa washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato kujitokeza kwa wingi na kuhudhuria sikukuu ya vibanda maarufu kama makambi 2017 ili waweze Yesu Kristo aweze kuwafumbua macho.

Akihubiri Kisa cha Wanaume wawili kutoka katika kitabu cha Luka 24 kuanzia mstari wa 13, ameeleza kuwa katika safari ya kutoka Yerusalemu hadi Emau, wanaume wawili waliambatana na Yesu ambaye alikuwa amefufuka, lakini kwa kuwa imani yao ilikuwa imekufa kutokana na kifo cha Yesu, hawakuweza kumtambua Yesu ambaye ni bwana na Mwokozi wa maisha yao. 
 Kwaya ya Shinyanga Mjini kutoka kanisa la Waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini


Amesema kuwa katika njia nzima Yesu aliwafundisha kwanza torati na ndipo alipokuwa akibariki chakula, Yesu aliweza kuwafumbua macho hawa wanafunzi wa Yesu na wakamtambua kuwa ndiye aliyekufa na kufufuka siku ya tatu.

  Kwaya ya Patmo kutoka kanisa la Waadventista Ndala

Mchungaji Tvuko amesema washiriki wa Kanisa waje walishwe maneno ya uzima ili waweze kufumbuka macho yao. Makambi ya mwaka 2017 yawe chachu ya kuharakisha uinjilisti wa neno la Mungu kwa kila mtu kujua habari njema ya ukombozi na kuwa tayari kwa ujio wa Yesu Kristo.

Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger