Wanachama wa chama cha vijana kanisani (AY- Adventist Youth) wakishusha ungo unakusanya mawimbi ya satelite,kwa lengo la kuamishia eneo lingine ambapo watalisimika kwa ajili ya kupata mawasiliano kutoka kwenye vituo vinavyorusha matangazo ya dini kama vile Morning Star Television, Morning Star radio na Hope Channel.
Kazi ya kushusha ungo unaonasa mawimbi ya sauti na picha za satelite ikiendelea.
Hapa ni mahali ambapo palionekana panafaa kwa ajili ya kupata mawimbi ya picha na sauti kutoka kwenye satelite. Hii imetokana na kutokuwepo na vikwazo vinavyochangia kuzuia mawimbi kama vile majengo marefu,miti n.k. Hapa vijana wanaonekana wakichimba shimo kwa ajili ya kusimika nguzo itakayobeba ungo wa satelite. Alievaa tshirt ya njano ni mkuu wa Idara ya Vijana kanisa la shinyanga mjini akiwa ndiye mkufunzi mkuu katika kutoa mada juu ya ufungaji wa dish kwa vijana wa kanisa.
Home »
» MAWASILIANO YA SATELITE
Post a Comment