Hawa ni baadhi ya washiriki wa kambi la Shinyanga Mjini wakijiandaa kuimba wimbo wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa makambi.
MOTTO: "WAABUDUO HALISI WATAMWABUDU MUNGU BABA KATIKA ROHO NA KWELI" Yohana 4:23-24
WIMBO MKUU: Namba 43 " Furaha Gani"
Kwaya iliyoalikwa ni: KASULU V.O.P
Mtaa wa Shinyanga Mjini una jumla ya makanisa matatu ambayo ni kanisa mama Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini, Ndala na Kizumbi
Kwaya ya Shinyanga mjini S.A.C wakiimba wimbo kabla ya mchungaji Tobe kuanza kuhubiri wakati wa ufunguzi wa sikukuu ya makambi katika mtaa wa Shinyanga mjini.
Mchungaji Tobe Kilalo, Mchungaji wa Mtaa wa Lubaga akifungua kambi la Shinyanga mjini mwaka 2015 kwa ujumbe wa kusimama dede wakati wote wa sikukuu ya makambi ili kila mshiriki wa kambi apate mibaraka kutoka kwa Mungu wetu wa mbinguni.
Mchungaji Tobe aliambatana na ubavu wake ambaye ni kama majuma matatu tu alipoachana na ubachala na kufanya agano la kuwa mme wa mke mmoja. Anayeonekana pembeni yake ni mke wake akiwa amehudumu kwa kusoma fungu kuu la somo la ufunguzi wa mkutano wa makambi.
Home »
» KUANZA KWA SIKUKUU YA VIBANDA MTAA WA SHINYANGA MJINI AGOSTI 9 2015





Post a Comment