Kanisa la Waadventista Wasabato Kanda ya Kusini mwa Ziwa Viktoria kwa kushirikiana na makanisa ya Waadventista Wasabato katika mji wa Shinyanga na vitongoji vyake, wanawaalika watu wote kwenye mikutano ya NENO LA MUNGU.
Mikutano hii itakuwa na kauli mbiu yenye ujumbe wa AMANI NA MATUMAINI MKOANI SHINYANGA kuanzia Jumapili ya tarehe 31 Mei hadi 21 Juni 2015 kuanzia saa 9:00 Alasiri hadi saa 12:00 jioni. Mikutano itafanyika katika vituo takribani 35 katika mji wa shinyanga ikiwemo Tambukareli, Tambukareli Mazinge, Bushushu Sokoni, Busushu B, Azimio, Matenkini, Shule ya balina Mwandui, Bubalaji, Mageuzi, Old Shinyanga, Kwajoni, Nhelegani Mashariki, Bugayambelele, Mwagala, Kambarage, Nguzo nane, Viwanja vya Shycom, Ibinzamata Mahakama ya Mbuzi, Bubale, Negezi, Ndala Bondeni, Busulwa, Bugweto Center, Jambo Ginnery, Magobeko, Ushirika Shuleni, Galamba, Matanda Mtengelani, Itilima, Masengwa, Iwelyangulu, Ilobashi, Ibadakuli center, Maganzo, Kolandoto, Mwadui, Mwamapalala, Dabaso, Mwakata, Mwakata Nhumbi, Mwigumbi, Mwasubi, Bunambiu, Bushola, Butuyu, Masunula, Ishinabulandi, Busanda, Tinde,
Mahubiri haya yataendeshwa na Mwenyekiti wa Jimbo la Kusini mwa Ziwa Mchungaji Joseph Buyengela akisaidiwa na Wachungaji na Wainjilisti. Baadhi ya Wachungaji na Wainjilisti ni Mch. Kwilasa, Mch. Kasika, Mch. Yusuph Mharagi, Mch. John Bomani, Mch Beautus Mlozi, Mrs Esther, Joseph Otieno, Mch Makunja, Paulo Shigela.
Mafundisho ya maisha ya Vijana na Malezi,pia elimu ya afya itatolewa. Kwaya mbalimbali kutoka ukanda wa kusini mwa ziwa zitatoa huduma ya uimbaji. Baadhi ya kwaya hizo ni Jangwani, Shinyanga Adventist Choir, Inalo Choir, Magu Choir.
Kupitia ukurasa huu tutawaletea matukio na matend makuu ya mibaraka kwa watu wa Mungu. nyote mnakaribishwa.
Post a Comment