Home » » KUTEGEMEZA UPENDO KATIKA VIPINDI VYA NDOA

KUTEGEMEZA UPENDO KATIKA VIPINDI VYA NDOA

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Wednesday, April 19, 2017 | April 19, 2017

WAZO KUU:
Katika injili ya kikristo kuna uwezekano wa kuwasaidia wanandoa kudumisha agano lao kati ya mabadiliko yanayoathiri ndoa zao. upendo uangaze.
‘Ni mpya kila siku asubuhi, uaminifu wako ni mkuu’ Maombolezo 3:23. ‘Nami nitakuposa kwa uaminifu, nawe utamjua Bwana’ Hosea 2:20

MABADILIKO NDANI YA NDOA
“Wanandoa wanaweza kupitia uzoefu wa mabadiliko kwa njia kadhaa.Jamii za KISASA hutegemea zaidi ndoa kwa namna ya uwenza, kutimizwa kwa mihemko, ukuaji wa wawili katika utambulisho binafsi”

BADILIKO LISILOTAZAMIWA
    Ni badiliko ambalo mtu hawezi kufanya maandalizi kabla ya tukio kutokea kama vile Vifo, maafa, magonjwa, kuhama kwa familia, hali ngumu ya kiuchumi, kupoteza ajira husababisha MISONGO  kadhaa katika mahusiano ya ndoa. 

BADILIKO LINALOTABIRIKA
    Ni badiliko ambalo mtu hufanya maandalizi kabla ya tukio kutokea na hii imechangiwa na kuwepo na somo la somo la maendeleo ya mwanadamu katika kipindi cha kabla ya kuzaliwa na kufa. Kwa jinsi ambavyo kuna vipindi katika maisha yetu, ndivyo kulivyo na vipindi katika ndoa zetu.
Vipindi katika ndoa hutokea kwa sababu ya mabadiliko ya mzunguko wa maisha kwa wenzi, lakini pia kwa sababu uhusiano una mzungukuko wake pia. Kila kipindi kina sifa kadhaa.
Nyakati wa kuhama kutoka katika kipindi kimoja kwenda kipindi kingine zinakuwa na uwezekano wa HATARI
Kufahamu mapema hatua hizi za maendeleo hutusaidia kujiandaa kuzikabili.





1.NDOTO: ‘Ninakupenda, lazima niwe na wewe, kamwe sitakuacha’.  Tofauti zilizopo zinavumiliwa, ugomvi huepukwa maana huaribu ndoto
2.Kuondoa kwa Fikra za Uongo: ‘Bado ninakupenda ila siwezi kuendelea bila badiliko, ninahitaji heshima’. Ndoto huanza kuyeyuka
3.Ugunduaji: ‘Ninakuona wa ajabu. Kile nilichopenda kwako hapo mwanzo nimetokea kukichukia’.
4.KINA: ‘Ninapokuwa na wewe hujisikia niko nyumbani, nimekamilika. Tunapotengana ninakuwa na amani na salama,tunapendwa’. Kuna mtiririko wa pamoja wa fikra za wanandoa.

Utafiti wa kitabibu unaonyesha ndoa ndani ya ndoa hudumu kwa muongo mmoja wenye vipindi vya mabadiliko kati ya wanandoa
Kushindwa kujadili kifungu katika ndoa ndani ya ndoa husababisha uwezekano wa talaka kutokea na kuzidi kufanya hali kuwa ngumu kwa mtindo wa kawaida wa ukuaji.

KUJITOA: Nguvu za kuimarisha katika nyakati za badiliko
Kama ndoa itafananishwa na maendeleo ya vipindi vinavyotokana na safari ya dunia kuzunguka jua, basi kujitoa kwa kila mmoja kwa mwezi wake ni sawa na nguvu ya uvutano inayoshikilia dunia katika mzunguko wake.
Kujitoa kwa mume na mke kila mmoja kwa mwenzake katika safari ya ndoa hutoa uhakikisho kwamba, lolote litakalotokea katika safari hiyo, WATABAKI WAMEJITOA KWA KILA MMOJA WAO.

Kila mmoja anapaswa kujifunza kumkubali mwenzi wake, pamoja na matatizo na mapungufu yetu.
Ndoa za Kikristo sio kujitoa kikamilifu tu, bali pia ni kukubali kujitoa, kujifunza kupenda na kuthamini mwenzi wako pamoja na udhaifu wake.
“Ndoa ya Kikristo ina umuhimu halisi inapobidi kukabili mabadiliko, kwa sababu imejikita katika agano la Mungu. Kipengele cha badiliko kinachoweza kuharibu hakiwezi kuathiri ndoa iliyoweka nanga yake kwa Mungu. Badiliko haliwezi kutisha upendo wa agano, bali husababisha badiliko, hutazama kilicho chanya ndani yake. Na hutumia mtazamo wa ubunifu. Upendo wa agano umejitoa kwa umilele, huvumilia mambo yote, huamini mambo yote, hutumainia mambo yote, hustahimili mambo yote. NI UPENDO USIOSHINDWA KAMWE”











Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger