Home » » RUHUSU MWANGA WA UPENDO UANGAZE

RUHUSU MWANGA WA UPENDO UANGAZE

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Tuesday, April 18, 2017 | April 18, 2017







WAZO KUU:
Kila wanandoa ambao ni wakristo, ni kitengo kinachohudumia, ambacho kinaweza kutumia upendo na umoja kama njia yenye nguvu ya kutangaza injili

Na kuinua maisha ya wanandoa wengine na hata mtu mmoja mmoja. Mwanzo 2:24; Yohana 13:34,35; 17:21; Waefeso 2:14
Kuna mtu yeyote ambaye hapendi kuhudhuria kwenye harusi? Kila kitu kuhusu harusi kimekusudiwa kutoa mvuto kuhusu ndoa;(mishumaa,maua,muziki, mavazi na hasa vazi la bibi harusi
Ndoa ni muhimu kwetu. Kila mwanandoa huwa na hamu ya kuonyesha hisia zake siku ya harusi.
Ndoa ya mwanadamu ni muhimu kwa Mungu. Ni mpango wa Mungu kwamba kila ndoa itoe tamko maalumu kwa dunia. Tamko hilo linatokana na upekee wa kila ndoa, na umoja wake.
Upekee wa kibiblia wa ndoa “MWILI MMOJA”.
Mwili mmoja una maana zaidi ya muunganiko wa kimwili wa mume na mke. Dhumuni ni wawe wamoja kiroho, wawe wamoja katika matumaini, pamoja na malengo na ndoto zao.

Mwanaume na mwanamke wana mwanzo mmoja. Hawa aliumbwa kutoka kwenye ubavu wa Adamu. Kwa hiyo Hawa anatoka katika malighafi ya udongo kama Adamu, hii inadhihirisha kwamba mwanamke hakupaswa kutawala kama kichwa wala kutawaliwa kama miguu bali alipaswa kusimama pembeni yake kama aliye sawa, ili apendwe na kulindwa nae.
Adamu anawakilisha mtu anayesubiri mwenzi. Kwa ujio wa Hawa, tofauti ya kijinsia ya binadamu inadhihirika. Mwanzoni Adamu alikuwa kiumbe mmoja na sasa wamekuwa viumbe wawili.
Wote kwa pamoja waliitwa kwa jina la ADAMU (mwanzo 5:2 kama ilivyo 1:26,27). Hapa pana dhihirisha kwamba umoja huu ulikuwa umekamilika. Ni baada ya anguko ndipo tunaposoma kwamba mwanamke anapewa jina la Hawa.

“Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako,na kuzaa kwako;kwa utungu utazaa watoto,na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala” (Mwanzo 3:16)
Anguko
    Katika anguko, Dhambi iligeuza asili ya mwanadamu. Uhusiano wa mume-mke ulibadilika. Laana ya dhambi ilileta laana kwenye mahusiano ya ndoa. PALE DHAMBI  INAPOTAWALA, NDOA HUTESEKA kutokana na UBINAFSI, nia ya kutaka KUJIRIDHISHA, na mazoea ya KUMNYONYA na KUMTAWALA mwingine.
Tamaduni mbaya katika ndoa
    Wanandoa wengi wanatamani kupata zaidi kutoka kwenye ndoa. Mara nyingi tamaduni mbalimbali zimehalalisha mifano isiyo sahihi ya ndoa, ambayo imekubalika na kuonekana ya kawaida.
    (SDA Bible Commentary, vol. 7, on Heb. 10:22)
Kutotumia Neema ya Mungu
    Kwa wale wasiotumia injili ya Neema ya Mungu katika mahusiano yao, ndoa zao hazichukui viwango alivyopanga Muumbaji wetu mwenye upendo.
Kukosa Mawasiliano
    Kukosa mawasiliano, au kwa kupigana na kulaumiana hali hii moyoni huzaa hisia za kukosa THAMANI na mtu anaweza kujitenga akijua au bila kujua kwa kuficha hisia.
Ubinafsi unasababisha tofauti za kawaida za kibinadamu katika umri, rangi, jinsia, mitizamo, tabia na mazoea yanayokuzwa.
Mara nyingi matokeo yake huwa ni kutokuelewana, hasira na migogoro. Jinsi tunavyozidi kuongea ubinafsi, ndivyo tunavyozidisha uwezekano wa kutokuelewana

Licha ya dhambi, Mungu hakutupilia mbali mpango wake wa asili wa mwanadamu kupata uzoefu wa ile hali ya ‘kuwa mmoja’ katika ndoa. Nia ya kimbingu kuhusu ndoa ni kwamba kila mwanandoa, hata baada ya anguko, kuhalalisha katika mahusiano yao hali hiyo ya kuwa ‘mmoja’ mwanzo 2:24.

“Kama ilivyo katika kila moja ya zawadi za Mungu alizowapa wanadamu, ndoa imechafuliwa na dhambi, lakini ni kusudi la injili kurudisha USAFI HUU na UZURI WAKE”


Wanandoa wachache sana wana mifano ya kuigwa ya ndoa za kudumu, zenye kujitoa na kuridhiana. Wachache zaidi wana marafiki wa kweli, sisi kama wanandoa wakikristo tunaweza kuwa marafiki wa namna hiyo.
Wanandoa wote hawana uzoefu unaolingana katika maisha yao ya kiroho.

“Wenye uzoefu wanatakiwa kuja kwa pamoja na kwa upole na unyenyekevu wa akili ili kushirikiana uzoefu wao. Uzoefu ulio hai, mpya na wa kuvutia unatakiwa kwa mkristo wa kweli. Uzoefu ulio hai unatengenezwa na mitihani ya kila siku, migogoro na majaribu, jitihata kali na ushindi, na amani kuu na furaha inayopatikana kwa Yesu.
Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger