WAZO KUU
Mungu alibuni ndoa ili kusaidia kukidhi haja za wanaume na wanawake katika muktadha wa uthibitisho, usalama, na ulinzi.
Kusudi la ndoa
1. Kuendeleza ukoo
Mwanzo 1:28, Zaburi 127:3

Ilikuwa ni mpango wa Mungu kwa ajili ya wanaume na wanawake kuungana katika
ndoa takatifu ili kupata watoto. Mahali ambapo kanisa la Mungu linapoumbwa ni katika upatikanaji wa watoto. Shetani akifanikiwa kuvuruga mwanaume au mwanamke katika ndoa, atakuwa amefanikiwa kuruga watoto na kanisa kiujumla. Vijana ambao hawajaoana wahakikishe hawavurugwi katika kuiendea ndoa.
2.Kuendeleza ukuaji wa Haiba na Neema

Mungu angeweza kuzidisha jamii ya kibinadamu kwa njia nyingine, kama alivyofanya kwa malaika. Kusudi la haraka ni kuendeleza na kupevusha haiba mbili tofauti katika uhusiano wa kushibana wa hawa wawili na majukumu. Ndoa ni kuunganika kwa watu wawili wa jinsia tofauti wanaoapa kuishi pamoja, kupendana, na kufanya kazi kwa pamoja kwenye mvua na kwenye jua, ugonjwa na afya, dhiki au baraka.
3. Kukuza uhusiano wa karibu
Kusudi la tatu ni kukuza uhusiano wa karibu na kuonyesha hisia kali zilizo sahihi kwa tendo la ndoa ambazo Mungu amejenga ndani ya wanadamu.1 Wakorintho 7:5
4.Kuwakilisha ndoa ya Kristo na kanisa
Uhusiano wa ndoa hakika ni uwakilishi au picha ya muunganiko wa Kristo na kanisa lake.
Post a Comment