WAZO KUU
Zawadi aliyotoa Yesu Kristo katika karamu ya harusi kule Kana ilikuwa ni ishara ya kile anachotaka kutufanyia katika ndoa zetu.
Fungu kuu:
Yohana 2:1-12
1. Hakikisha unamwalika YESU katika ndoa zetu. Yeye ana uwezo wa kufanya kwa ubora wa juu.
2. Fanya kile anachokuambia
3. Toa vilivyo vyema zaidi.
Uzoefu na takwimu vinadhihirisha kwamba huu upungufu wa divai bahati mbaya hujitokeza katika ndoa nyingi hata leo. Sisi ni binadamu, hatuwezi kuishi bila ukomo wa rasilimali chache za kibinadamu tulizo nazo.
Matatizo yanaweza kuwa makubwa au madogo. Tofauti ya ndoa za Kikristo na zile za kidunia ni moja. Katika ndoa za Kikristo, Yesu ni wa kwanza katika orodha ya wageni.
Leo Yesu anataka kutupatia mahitaji yetu na kututatulia matatizo yetu. Naye anataka kufanya zaidi kuliko mipaka na matarajio ya kibinadamu. Fanya kila atakachokwambia.
Post a Comment