Mwalimu Ibrahimu Magoma |
WAZO KUU:
Uhusiano wa karibu wa mume na mke katika ndoa unawasaidia kujisheheni kwa namna iliyobora zaidi kukabiliana na kustahimili zahama ambazo zinaweza kuandamana na maisha.
Kwa miaka mingi, ndoa imekuwa na maana mbalimbali kwa watu tofauti. Nyakati zote ndoa imekidhi kusudi la kuunganisha pamoja jamii mbili, mataifa mawili au makundi mawili (mwanzo 34:9,10,16).
Ndoa kwa wengine imekuwa ni njia tu ya kupata watoto kihalali ili kuendeleza jina la familia (mwanzo 30:3-5), wengine wameoana kwa sababu ya kupata wasaidizi, usalama, kiuchumi, utegemezi au kupata hadhi katika ndoa (mithali 31:10-29). Uchu wa ngono imekuwa sababu nyingine inayosababisha watu kuingia katika mahusiano ya ndoa (Waamuzi 14:2-3; 2 Samweli 11:2-4).
MWILI MMOJA: UTAMBULISHO WA WAWILI
Mwalimu Ibrahimu Magoma |
Kwenye kiini cha mpango wa kimbingu wa ndoa kuns kulea, na kutegemea kiroho na kumhemuko kunakoletwa na kila mmoja wa wenzi kadiri maisha yao yanavyounganika pamoja. Kote katika maandiko tunapata ile hali ya umoja, maisha ya njozi iliyopo katika ndoa yakielezewa kwa mitizamo tofauti lakini yakiunganika kutupatia uelewa wa mpango wa Mungu kwa ajili ya huo umoja katika ndoa.
NDOA KAMA UBIA
Maelezo ya ndoa ya kwanza yalifuatiwa na kitendo cha mbingu kutambua kwamba mwanadamu alikuwa mpweke. "Bwana Mungu akasema, si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye." (Mwanzo 2:18). Msaidizi ni yule mtu aliye tayari kutia kutia moyo na kuimarisha katika upeo wa kibinadamu kwa jinsi ambayo Mungu anatusaidia na kututegemeza kama msaidizi wetu kimbingu.
Darasa la watoto wa miaka 0-3 |
Wazazi na Watoto wenye miaka 0-3 katika darasa lao wakijifunza somo la upendo kama mvulana Daudi alivyopenda kondoo aliokuwa akiwachunga |
Post a Comment