Home » » NDOA YAKO: JINSI INAVYOJENGA KIZAZI KIJACHO

NDOA YAKO: JINSI INAVYOJENGA KIZAZI KIJACHO

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Thursday, April 20, 2017 | April 20, 2017

WAZO KUU:
Pale Roho wa Kristo anapokaa ndani ya moyo wa mume na mke, ndoa yao inaweza kuwa mvuto mkubwa wa kujenga maisha ya watoto wao na kuwaongoza kuelekea kwenye maadili chanya.

Waefeso 5:25, Tito 2:4 na Kumbukumbu la Torati 6:6-7

Kujenga uhasama, matusi na mambo kama hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa wanandoa kuvunjika moyo. Lakini Yesu Kristo anawafariji wanandoa waliovunjika moyo. Roho wa Bwana hufufua tena hisia za faraja kwa wenzi ambao wana nia ya kuanza maisha yao upya.

Kwa sababu neema ya Kristo inauwezo wa kuimarisha na kuboresha kile ambacho Shetani alichokiharibu katika ndoa takatifu. Ni nini umuhimu wa ndoa ya Kikristo kwa mafundisho na maisha ya watoto?

Kama watoto wataona upendo kati ya baba na mama, wataelewa kuwa baba na mama wanapendana. Umuhimu wa upendo utajengwa katika maisha ya watoto. Utiifu wa watoto utaonekana kuanzia nyumbani hadi kanisani. Na kizazi chao kitakuwa na faida kwa maisha yao.

Katika familia yenye wazazi wawili mahusiano mazuri ya wazazi yana mvuto kwa watoto na hujenga kuimarisha mahusiano ya watoto wao kwao, wazazi kwa watoto na watoto kwa jamii nzima. Upendo wa wazazi unafananishwa na mfumo wa joto nzuri ndani ya nyumba ambapo watoto hawatasikia baridi.

Wazazi wenye upendo na uchangamfu huchangia watoto kujifunza mambo mazuri, huchochea kasi ya kujifunza katika masomo na pia hujenga ujasiri na kujiamini. Upendo wa wazazi husaidia watoto kuamini wazazi na kuamini taarifa yoyote itakayotoka kwa wazazi.

Matendo yanayostawisha upendo ni yapi?
1. Maneno yenye upendo na shukrani
2. Ujumbe unaondikwa kwa wenzi na kusomwa mbele ya watoto.
3. Kupeana Zawadi kwa wenzi 

Kama wazazi wangejikita sana kwa hisia za watoto, ukuaji wa watoto ungefurahiwa katika kipindi chote cha ukuaji wa watoto. Mfano tunapowabeba watoto wetu katika mapaja husaidia kumjengea mtoto kuwa na ufahamu wa kujali wengine.

Kutokuheshimiana kwa wazazi kuna athiri kwa kiasi kikubwa ukuaji wa watoto kimaadili. Huchangia kwa asilimia kubwa kizazi cha watoto hao kutokuwa na ndoa yenye manufaa wakati watakapokuwa tayari kuingia katika taasisi yao ya ndoa.


















Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger