Home » » UIMBAJI UNA NGUVU ZAIDI YA BOMU LA ATOMIC

UIMBAJI UNA NGUVU ZAIDI YA BOMU LA ATOMIC

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Sunday, April 02, 2017 | April 02, 2017

Katika Picha kuanzia kushoto ni Dr Maeja(Mwakilishi wa Mgeni rasmi), Mchungaji Kilinda J(Mchungaji wa Mtaa wa Shinyanga Mjini), Mr.Sengoka Mdambi, Mr. Amani Tibore na Mr Songola (Wazee wa Kanisa)
Hatimaye yametimia ambapo Mchungaji wa Mtaa wa Shinyanga Mjini Mch. Kilinda J alipoongoza waumini katika mitaa yote ndani ya Manispaa ya Shinyanga kuibariki kazi nzuri ya kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini.

Kabla ya kuibariki kazi iliyopo ndani ya DVD namba 3 yenye jumla ya nyimbo 10, kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ndugu Magoigwa, mzungumzaji aliyemwakilisha mgeni rasmi Dr Maeja alitoa ujumbe wa mgeni rasmi kwa kutoa mchango wa Tsh 1,000,000.

Dr Maeja alielezea kwa kina ujumbe mkuu uliopo katika mkanda huu wa DVD kuwa umebeba jina la "Ni Jambo Gani Gumu?" kuwa utunzi wa ujumbe huu umetokea katika vitabu vya Mwanzo 18:14, Yeremia 32:17 na Zakaria 8:6
Dr Maeja akizungumza na Waumini waliohudhuria tukio la kuitambulisha na kuibariki DVD namba 03 ya SAC


Wakati huo huo Mchungaji Kilinda alinena na waumini kwa kusisitiza maandiko yanavyosema juu ya namna ya uimbaji kuwa uimbaji hauna budi kuonyesha shangwe na furaha (Zaburi 71:22-23). Aliendelea kusema kuwa uimbaji ni lazima ulete amani kwa watu wa Mungu kwa sababu muziki  ulianzishwa kwa makusudi ya kutoa huduma na kwa makusudi matakatifu, kwa hiyo chochote kinachofanywa na waimbaji ni vema kiwakumbushe watu kuwa katika ibada ya kumuabudu Mungu na si vinginevyo. Ujumbe wa mchungaji Joram Kilinda unaweza kuupata kwenye hii linki ya youtube wakati yakirushwa live (Picha hazionekani, utasikia sauti tu)
Mchungaji Kilinda akihubiri namna uimbaji ulivyo na nguvu zaidi ya bomu la atomic

Kwaya mbalimbali zilihudhuria katika kutoa ushirikiano kwa kwaya ya SAC (Shinyanga Adventist Choir). Kwaya ambazo ziliweza kuimba katika tukio hili ni kwaya kongwe katika ukanda huu wa ziwa viktoria na Tanzania (Jangwani SDA Choir) kutoka katika kanisa la Waadventista wa Sabato Ushirika na kwaya ya Kanisa la Ndala.
Jangwani SDA Choir

Ndala SDA Choir
Wenyeji ambao ni Kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini (SAC-Shinyanga Adventist Choir) waliweza kuimba nyimbo zilizopo katika DVD namba 3 kwa utukufu wa Mungu. Unaweza kufuatilia kupitia youtube shughuli nzima ilivyokuwa ikirushwa live (audio) kupitia link hii.
Shinyanga Adventist Choir

Shinyanga Adventist Choir

Shinyanga Adventist Choir

Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger