Home » » UZOEFU WA KILELENI:FURAHA YA KWELI INAPATIKANA KILELENI

UZOEFU WA KILELENI:FURAHA YA KWELI INAPATIKANA KILELENI

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Tuesday, April 11, 2017 | April 11, 2017

Mchungaji Keshi Martin Malehiwa
"Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo,hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko.Bwana akamwonyesha nchi yote. Bwana akamwambia hii ndiyo nchi niliyowaaapia Ibrahimu na Isaka na Yakobo,nikisema nitawapa wazao wako. "Kumbukumbu la Torati 34:1-4

Mifano ya uzoefu wa kileleni ktk biblia
Katika biblia vilele vya milima vimeelezwa kama mahali ambapo Mungu alijifunua wazi na kuonyesha utukufu wake na kufanya ushirika na mawasiliano ya karibu sana pamoja na watu wake.

i)Katika kilele cha Pisga,Mungu alimuonyesha Musa nchi ya ahadi(kumbukumbu 34:1)
i)Katika kilele cha mlima Horebu Mungu alizungumza na Eliya(1falme 19)
ii)Katika kilele cha mlima Moria Mungu alijifunua na kuzungumza na Ibrahimu (Mwanzo 22)
iii) Katika kilele cha Mlima Karmeli Mungu alijibu maombi ya Eliya(1falme 18)
iv)Katika kilele cha mlima Sinai Mungu alizungumza na Musa kama na rafiki yake(kutoka 24:16)
v)Katika kilele cha mlima wa Mizeituni,,Yesu alibadilika sura na Petro Yakobo na Yohana wakauona utukufu wake(Luka 9)

Maana ya Kiroho ya uzoefu wa kileleni
☞Ni neema ya Mungu ya kuinuliwa kiroho na kiakili na kuketishwa katika utukufu wa Mungu,kufanywa kuwa rafiki wa karibu na Mungu na kuonyeshwa uzuri na fahari ya makao ya milele baada ya maisha haya.(Waefeso 2:6)
☞Ni kuishi duniani ukiwa mbinguni,ni kutembea pamoja na Mungu kama Henoko(Mwanzo 5:24)
Maisha ya watu waliofika kileleni pamoja na Mungu

Wameinuliwa kiakili na kiroho na kuketishwa katika utukufu wa Mungu,wamenza kuonja ufalme wa Mungu kuanzia sasa(luka 17:21)
Wanaishi mbinguni wakiwa duniani(wamehamishwa kiroho na kiakili)-Waefeso 2:5-6,Wakolosai 3:1-2
Wanaongea na kutembea na Mungu kama rafiki yao(Kutoka 33:11)
☞#Wanaishi kwa imani,si kwa kuona,wana macho ya ziada,wanaona vile wengine hawawezi kuona (2wakorintho 5:7)
Wanajua na wanaishi kama wasafiri na wapitaji ktk dunia hii(Waebeania 11:13)
Wameiona nchi ya ahadi; nchi mpya,mbingu mpya na Yerusalemu mpya,makao waliyoandaliwa,dunia iliyofanywa upya,bustani ya Mungu,hakuna magonjwa,wala kifo,wala maumivu,wala vilio,wala vilio,ni furaha milele zote,mambo ya dunia hii kwao ni mambo yanayopita(Kumbukumbu 34:1-4)
Wanaijua familia kubwa watakayoishi,wote watakaokombolewa,hakuna kuachana,hawakati tamaa kwa changamoto za familia wanazozipitia sasa,maana ni za kitambo tu.(1Petro 2:9)
Hawana msongo,wala mfadhaiko,wamejaa matumaini,hata katika misukosuko(Yakobo 1:2)
Kila siku wanabadilishwa kufanana na Mungu.(1Petro 1:19)
Hawaogopi chochote,hata kifo,maana wana Mungu(Luka 12:4)

Kwa ujumla waliofika kileleni pamoja na Mungu,wanaishi katika ufalme wa Mungu wakiwa hapa duniani.Umasikini,magonjwa,kutengwa,na changamoto za maisha haya haziwanyimi furaha wala kuwatenga na Mungu,maana ni za kitambo tu
Paulo alipofika kileleni pamoja na Mungu,aliyahesabu mambo ya dunia hii kuwa sawa na mavi(wafilipi 3:8)
Martin Luther King alisema"nimekuwa katika kilele cha mlima,na nimeiona nchi ya ahadi....na sasa siogopi chochote..."

Tunafikaje kileleni pamoja na Mungu?
☞Soma neno la Mungu kila siku,ni biblia pekee inayomfunua Mungu na fahari alizotuandalia kileleni(Waebrania 4:12)
☞Omba mara nyingi kwa kadri uwezavyo:Maombi ndiyo njia pekee ya kujenga uhusiano wa kudumu pamoja na Mungu(1Thesalonike 5:17)
☞Tii kila anachokuagiza Mungu katika neno lake:Utii ni bora kuliko sadaka yoyote unayoweza kumtolea Mungu.(1Samweli 15:22)
Karibu kileleni pamoja na Mungu

Mpendwa msomaji,haidhuru unapitia uzoefu wa kukatisha tamaa kiasi gani, bado hujachelewa kufurahia uzoefu wa furaha kileleni ukiwa pamoja na Mungu.

Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger