Vijana wa chama cha Mabalozi na chama cha watafuta njia kutoka kanisa la waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini,walifanya ziara ya kutembelea jengo linalojengwa kwa ajili ya matumizi ya kutoa huduma ya kitabibu kwa wanadamu. Siku hiyo vijana hao walichangia mifuko 5 ya cement kama mchango wao kufadhili ujenzi wa jengo hilo. Baada ya zoezi la kukabidhi mifuko ya cement kwa mwenyekiti wa Jimbo la kusini mwa Nyanza (Aliyevaa Koti), vijana waho walielekea visiwa vya Sanane kwa ajili ya kujionea uumbaji na maajabu ya uumbaji.
Vijana wakipewa ushauri wa kusoma ili waje walitumikie kanisa na taifa kwa uzalendo.Mojawapo ya ushauri waliopewa ni kuwa mahali hapo walipotembelea watakuja kama wataalamu waliobobea katika fani zao mbalimbali. Na iwapo wasipojitahidi kusoma hawataweza kwenda pale kufanya kazi ila wataenda pale kutibiwa wakiwa wagonjwa.
Home »
» MABALOZI NA WATAFUTA NJIA WAFANYA ZIARA YA KUCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI YA PASIANSI
Post a Comment