NAFASI YA KAZI (MWALIMU MKUU)
Tunapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa kanisa la Waadventista wa Sabato Shinyanga Mjini linategemea kuanzisha shule ya awali na shule ya msingi katika Manispaa ya Shinyanga mapema Januari 2016 iitwayo EDEN PRE-PRIMARY & PRIMARY ENGLISH MEDIUM SCHOOL.
Tunawaarifu kuwa shule yetu ya chekechea iliyoanza mwaka 2008 itaendelea kuwa maeneo ya kanisa la wasabato Shinyanga Mjini.
Ili kufanikisha lengo, kanisa linatangaa nafasi ya Mwalimu mkuu mwenye sifa zifuatazo:
1. AWE MCHA MUNGU, MWAMINIFU, MTIIFU,MBUNIFU,MCHAPAKAZI
2. AWE NA UWEZO WA KUONGOZA, MSHIRIKISHAJI.
3. AWE NA STASHAHADA YA ELIMU AU CHETI CHA UALIMU DARAJA LA IIIA
4. AWE NA UZOEFU WA KUFUNDISHA ENGLISH MEDIUM SCHOOL
5. AWE NA UWEZO WA KUFUNDISHA NA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA.
Mshahara na maslahi mengine ni stahili sahihi kwa utumishi huu kwa kutegemea sifa za mwombaji, majadilianomnna makubaliano yenye tija kwa pande zote mbili.
Kama unazo sifa tajwa hapo juu, tuma maombi yako mapema kabla ya 18.12.2015 saa 7:00 mchana kwa :
KATIBU WA BODI
EDEN PRE-PRIMARY & PRIMARY ENGLISH MEDIUM SCHOOL
P.O.BOX 106
SHINYANGA
Simu: 0713544355
Post a Comment