Home » » RAIS TED WILSON KATIKA UIMBAJI

RAIS TED WILSON KATIKA UIMBAJI

Written By SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH on Sunday, April 09, 2017 | April 09, 2017

Rais wa Kanisa la Waadventista wa Sabato duniani Mchungaji Ted N.C. Wilson amekuwa mfano kwa jamii ya waumini wa kanisa la Waadventista wa Sabato kwa kuendelea kumtukuza Mungu kwa kuimba. Katika wimbo wa "Tell Someone About Jesus"(Mwambie mtu fulani kuhusu Yesu), Mchungaji Ted Wilson anaonekana akiimba kwa furaha sana akidhihirisha kujitoa kwake kumtangaza Yesu Kristo.

Katika ujumbe wake katika akaunti yake twitter amekaririwa akisema kwa neema, Mungu amegawa vipaji kwa kila mmoja wetu, tumuombe atuonyeshee njia nzuri ya kuvitumia vipaji kwa ajili ya huduma zake. 

Katika kujifunza kumtumikia Mungu, mchungaji Ted Wilson anakumbusha waumini kuwa vitu vyote tulivyonavyo ikiwemo muda, mali na miili yetu ambayo imebeba vipaji mbalimbali  ni mali ya Mungu. Tuendelee kuomba kila wakati Roho Mtakatifu atukumbushe tumtukuze Mungu na tusije tukajisifu kupitia vipaji hivyo.

Jambo la muhimu ni kujiuliza tuna nini mikonni mwetu na tukishagundua tulichonacho tuweze kuvikabidhi vyote katika mikono ya Mungu ili aweze kutuelekeza njia sahihi ya kuvitumia vitu vyote alivyotupatia.

Mibaraka ya kipekee "supernatural blessings" zinatokana na rasilimali tulizonazo mikononi mwetu. Mara tu baada ya kumkabidhi Yesu Kristo ile mikate mitano na samaki wawili iliyokuwa katika mikono ya wanafunzi wa Yesu, wanafunzi wa Yesu na makutano walishuhudia miujiza na mibaraka ya ajabu ya kuwalisha watu elfu tano na chakula kikabaki (Mathayo 14).

Kutazama Mchungaji Ted Wilson akiimba  "Tell Someone About Jesus" tazama kwenye VIDEO ZETU MBALIMBALI au bonyeza hapa.

BWANA AKUBARIKI

 Tell Someone About Jesus
Verse 1 
Go tell someone about Jesus! Be swift His command to obey 
Proclaim unto all His salvation, Go now, and no longer delay 

Chorus 
Tell someone about Jesus, Many are waiting to hear 
Many are sad and discouraged, Tell them the story so dear 

Verse 2 
Go tell someone about Jesus! Go tell of His wonderful love 
Go tell how He came from His glory The home of the Father above 

Verse 3 
Go tell someone about Jesus! Bring souls out of darkness to light 
From byways and highways go lead them To paths that are sunny and bright 




Share this article :

Post a Comment

 
Need Support? Contact : Creating Website and Blog | Stanley Isaac Manyonyi | Twitter
Copyright © 2017. SHINYANGA CENTRAL SDA CHURCH - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger